BurudaniUncategorized

Kutana na mtoto ‘Ryusei Imai’ anaedaiwa kuwa mrithi wa Bruce Lee ni noma!! (+Video)

Hakuna ubishi kuwa Bruce Lee ni moja ya watu maarufu waanzilishi wa Martial Arts duniani na kifo chake wataalamu wengi wanasema pengo la kifo chake halitowezi kuja kuzibika kwa muda mrefu.

Picha inayohusiana
Bruce Lee

Kuna watu wengi wamejitahidi kufuata nyayo zake lakini bado hawajafikia hata nusu ya uwezo wake hii ni kutokana na kiwango alichokuwa anakionesha kwenye uhalisia wa maisha yake hasa hasa mazoezi makali na ubunifu wa Movie zake.

Sasa hiyo inaweza ikawa ni historia tuu kwani tayari wadau na wafuatiliaji wa mchezo wa Kung Fu wamempata mtoto mmoja wa kijapani aitwaye, Ryusei Imai mwenye miaka (6) tu ambaye huenda akavaa viatu vya Bruce Lee kutokana na uwezo wake anaouonesha kwasasa.

https://youtu.be/RLPPEAgwri0

 Mtoto Ryusei Imao (6) ambaye ni mzaliwa wa Kanagawa nchini Japan umaarufu wake ulianzia kwenye mitandao ya kijamii baada ya mzazi wake kuposti video fupi kwenye mtandao wa facebook na watu kibao kupenda video hiyo.

Mtoto huyo mwenye muonekano wa kikakamavu tayari ameanza kutabiriwa kama mrithi wa Bruce Lee kwani ameanza kuonesha muelekeo wa kuchukua mikoba ya mkali huyo.

https://youtu.be/aeyWPiogUZs

Bruce Lee amefariki mwaka 1973 na kuacha filamu kama Game of Death (1978 posthumous), Enter the Dragon (1972),The Way of the Dragon (1972),The Chinese Connection (1971) na The Big Boss (1971).

Tusubiri kuona mtoto huyo kama ataweza kuvaa viatu vya Bruce Lee kwenye duniani hii yenye kila aina ya vipaji .

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents