Burudani

‘Kwanini umefanya hivyo?’ Mtoto wa miaka 8 amwandikia barua Justin Bieber

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane ameandika barua ya wazi kwa Justin Bieber akimuuliza ‘Kwanini umefanya hivyo’ kufuatia kukamatwa kwake na polisi jijini Miami.

Bew9XiOCYAAWfjk

Serafina, kutoka Ohio, amesema amefedheheshwa sana na muimbaji huyo mwenye miaka 19 na kumwambia: Nadhani unatakiwa kufedheheshwa na wewe mwenyewe. Chukua muda na fikiria ulichokifanya.”

Mama wa mtoto huyo, Ami amesema mwanae huyo amekuwa shabiki wa Bieber tangu akiwa na miaka mitatu.

Bieber aliachiwa kutoka alikokuwa ameshikiliwa baada ya kutoa dhamana ya $2,500. Anakabiliwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa, kuvuta bangi na kuwa na leseni iliyopitwa na muda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents