Burudani

Lameck Ditto atajwa kuwania RFI-France 24 Discoveries Award 2012

Muimbaji wa THT, Lameck Ditto amekuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki na Kati, kutajwa kuwania tuzo za mwaka huu za RFI-France 24 Discoveries.

Jumla ya wanamuziki kumi barani Afrika wametajwa kuwania tuzo hizo.

Bongo5 imezungumza na Ditto kutaka kujua hatua alizopitia mpaka kutajwa kuwania tuzo hizo.

“Hizi unajua zinatokana na jinsi wewe unavyotuma kazi zako katoka Radio France International na France 24 ni TV ambayo wao wanahusika nayo kwa asilimia kubwa. Kwahiyo pale huwa wanatoa taratibu zao wao wenyewe, wakishatoa wewe unawasiliana nao, ukishawasiliana nao wanacheck but wanapataga watu wengi, watu kama elfu 20, 25 hivi. Kwahiyo wao wenyewe wanakuja wanatafuta mwisho wanapata mtu mmoja ambaye wanamkabidhi hiyo tuzo na East Africa mtu wa mwisho kuleta hiyo tuzo ni Maurice Kirya na imemsaidia sana,” alisema Ditto”

“Zinatolewa Paris Ufaransa na ni December 6 but kura ni siku kumi tu zimetolewa kwaajili ya kupiga kura. Ni tuzo muhimu na kubwa sana Afrika. Unajua ukubwa wa Radio France International, unajua ukubwa wa France 24 ni TV kubwa sana kwa Ufaransa ndio idhaa yao ya taifa na mshindi anapata vitu vingi sana ukiacha mifedha lakini pia kuna mkataba wa kufanya tour dunia nzima pia kuna package ya promotion kubwa sana kwasababu wao lengo lao ni kusupport wanamuziki kutoka Afrika.”

Ditto alielezea pia jinsi ya kumpigia kura ili aweze kushinda tuzo hizo, “kura unapiga kwa kwenda kwenye website yao ya www.rfimusic.com, ukishafika pale utakuta RFI-FRANCE 24 DISCOVERIES AWARDS 2012 unaclick katika ‘vote for your favorite Artist before September 24th’, unaenda katika comments pale unawaambia kwamba mimi msanii wangu ambaye nataka ashinde ni Lameck Ditto from East Africa. Afrika nzima katika upande wetu huku nimetoka mimi tu but napambana na watu kutoka Nigeria, Senegal, Namibia na wapi, lakini huku Afrika Mashariki nipo mimi tu.”

Mwanamuziki huyo amewasisitiza wananchi wampigie kura ili awe kuutanganza muziki wa Tanzania, “unajua hii ni habari njema katika muziki wetu na ni kitu ambacho kinatoa nafasi ya sisi muziki wetu kukua zaidi kwasababu endapo mimi nitapata ile tuzo itakuwa milango imefunguka kwangu, kwa watu ambao niko nao kila siku, kwasababu ninapopata mimi tour ya kuzunguka labda dunia nzima kufanya performance ni kwamba mimi natangaza muziki wetu, natangaza nchi yangu, natangaza muziki wetu unazidi kukua watu wanazidi kutufahamu zaidi. Maurice ile tuzo ambayo ameipata imemtambulisha dunia nzima yaani sasa hivi kafanya festivals nyingi watu wengi wanamjua show kwake zimekuwa nyingi tena zile show kubwa kubwa. Na mimi lengo langu la muziki ninaoufanya nafika huko sababu ni njia ambayo mimi nataka kupita. Njia ambayo mimi nataka kupita ni kuwa musician mkubwa wa Afrika ambaye anatokea Tanzania, kila siku nazungumza hicho kitu. Kwahiyo wanipigie kura ili kusupport hicho kitu ambacho mimi nafikiria, tufanikiwe kufikisha muziki wetu katika level ambayo kila mtu atauheshimu.”

Wasanii wengine wanaowania tuzo hizo ni pamoja na Elemotho, (Namibia), GT the Guitarman (Nigeria), Denis Larose (Mauritius), Nasser (Mauritania), Maryse Ngalula (DRC), Spyrow (Côte d’Ivoire), Takeifa (Senegal) na Anonyma (Senegal).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents