HabariMichezo

Ligi yetu kuna mahali tumefika, sio tulipotoka – Naibu Waziri Mwana FA

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Naibu Waziri wa Michezo Sanaa na Utamaduni Hamis Mwinjuma alimaarufu @mwanafa ameelwza namna Ligi kuu ya Tanzania ilivyopiga hatua kwa Afrika Nzima.

Ameandika kuwa “ Kuna mahala tumepafikia na mpira wetu. Bado tuna safari ya kufanya mambo ya hivi kuwa YA KAWAIDA, ila hatupo tulipokuwa.
Asante sana Mwanamichezo namba moja nchini Mhe Rais Dkt @samia_suluh_hassan kwa kuwa na moyo wa kuunga mkono juhudi za vijana wako bila kuchoka, unawapa sana moyo wa kuongeza juhudi na matokeo yanaonekana.
Asanteni sana @yangasc na@simbasctanzania kwa msimu
huu muri kuliko yote tuliyowahi kuwa nayo Afrika. Twendeni nusu fainali sasa rekodi zinyooke zaidi. Ushindani wenu una faida kubwa kwa nchi yetu”

Ikumbukwe kuwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Tanzania ndio nchi pekee imeingiza timu mbili kwenyw Robo Fainali ya michuano hiyo ambazo ni Simba na Yanga na hii ni kwa mara ya kwanza kutokea nchini.

Bofya hapa kusoma zaidi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents