Habari

Linex aukusanya mkwanja alioupata kwenye muziki kujenga ‘lodge’ kwao Kigoma

Hitmaker wa Mahakama ya Mapenzi, Linex Sunday Mjeda, amefunguka kwa kusema mkwanja aliokusanya kwenye muziki ameupeleka Kigoma ambako anajenga lodge ya biashara.

_7_full

Akizungumza na Bongo5 leo, Linex amesema alichohitaji kuvuna katika muziki wake kwa mwaka 2013 kimetimia kwa asilimia 80.

“Sasa hivi nina project ya kujenga Lodge Kigoma. Kuna kiwanja, mawe na kila kitu,nguvu yake imetafutwa mwaka huu,kwaHiyo mwakani ni kufanya au kutekeleza, sitaki kuupeka harahara kwasababu ni wa fedha nyingi ambao nikiupeleka haraka haraka kUtaniyumbisha kimaisha,” amesema.

“Nilikikuwa na ndoto ya kujenga nyumba ya biashara ambayo itaweza kuniingizia fedha nikaishi daima milele na milele mpaka Mungu atakaponichukua,ingawa sijajua ujenzi utachukua muda gani mpaka kumalizika, ila Mungu anipe uzima umalizike mapema.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents