Burudani

Linex kufunga mwaka na wimbo mpya ‘Salima’ aliomshirikisha Diamond

Msanii wa muziki Linex Sunday Mjeda amefunguka kwa kusema kuwa anafunga mwaka kwa kutoa wimbo ‘Salima’ ambao amemshirikia Diamond.

Linex

Akizungumza na Bongo 5 leo, Linex amesema audio ipo tayari na wanachomalizia sasa hivi ni maandalizi ya video ambayo wanafanya na Adam Juma.

“Kabla mwaka haujaisha inabidi tufunge mwaka na wimbo ambao nimefanya mimi na Diamond ambao umeshalipiwa video, sema sasa imeshindwa kumalizika ndani ya muda kwa sababu kila mmoja anakuwa kwenye mihangaiko yake, kwahiyo wimbo unaitwa Salima amefanya Tuddy Thomas na videoa atafanya Adam Juma,” alisema Linex.

Katika hatua nyingine Linex ametoa deal kwa msichana yoyote ambae anaweza akawa model ndani ya video hiyo mpya.

“Tunahitaji msichana wa mjini ambaye anaweza akabadilika na kwenda kwenye mwonekano wa kijijini, ni msichana wa mjini lakini tumbadilishe awe kwenye mwonekano wa kijijini, ndiyo maana tumekwambia tunamtafuta.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents