Burudani

Linex kutupa karata yake kwenye muziki wa gospel

Msanii wa muziki, Linex Sunday Mjeda, amesema taachia wimbo mmoja wa gospel ili kutoa burudani tofauti kwa mashabiki wa muziki wake.
Linex

Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni aliachia wimbo ‘Hewala’akiwa amemshirikisha Christian Bella, ameiambia Bongo5 Jumanne kuwa wimbo huo utatoka audio pamoja na video.

“Mwaka huu bado kuna ngoma nyingi zinakuja, tutaangalia ratiba inasemaje lakini mwezi Disemba nitaachia wimbo wa gospel, audio na video, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna mambo mazuri yanakuja,” alisema Linex.

Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya video yake ya wimbo ‘Hewala’ aliyomshirikisha mfalme wa masauti Christuian Bela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents