Habari

Lowassa afunguka kuhusu mgogoro unaoendelea CUF

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amevunja ukimya kuhusu mgogoro wa uhalali wa Uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa unaoendelea ndani ya chama cha wananchi CUF.

Lowassa ambaye alitajwa na Profesa Lipumba kuwa chanzo cha yeye kujiuzulu kabla ya kurejea tena miezi tisa baadaye kutengua uamuzi wake, amesema kuwa kushindwa kwa chama hicho ni kushindwa kwao na vyama vyote vinavyounda UKAWA.

Mjumbe huyo alitumia ukurasa wake wa Facebook kueleza jinsi ambavyo Ukawa inalibeba tatizo la mgogoro unaendelea ndani ya chama cha CUF. “CUF ni wenzetu katika Ukawa. Shida zao ni shida zetu, vita vyao ni vita vyetu, kushindwa kwao ni kushindwa kwetu, ushindi wao ni ushindi wetu,” aliandika Lowassa.

Profesa Ibrahim Lipumba amekuwa akieleza kuwa hayuko tayari kuona Chadema au Lowassa wanakinunua chama hicho.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents