Habari

Lowassa awapongeza Wamarekani kwa kumchagua Donald Trump

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa,Edward Lowassa, amewapongeza raia wa Marekani kwa kumchagua Donald Trump kuwa rais mpya wa nchi yao.

Hayo yamesema na Mjumbe huyo, Jumapili hii katika misa maalumu ya shukrani ya mwaka mpya 2017 iliyoshirikisha madhehebu mawili ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli na kanisa Katoliki, wilayani Monduli, mkoa wa Arusha.

“Wamarekani hawakufanya makosa kumchagua Trump kwani anaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza taifa hilo tajiri duniani ambalo linategemewa na mataifa mengine, dunia imebadilika amechaguliwa rais mmoja huko Marekani ambaye ni mwamba kweli kweli,’ alisema Lowassa.

“Hatuwezi kumtabiri mambo yake yatakavyokuwa, lakini inabidi kila mtu afanye kazi kwa bidii na kwa maarifa kwa sababu huyo hakubali upuuzi wowote.”

Lowassa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Monduli kwa miaka 20, aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika kwani hiyo ndiyo njia iliyo sahihi ya kuweza kuondokana na umaskini.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents