Burudani

Mabeste adai hawezi kujuta kujichora tattoo ya jina la mpenzi wake

Rapper Mabeste amesema ataendelea kubaki na tattoo ya jina la mpenzi wake Lisa hata kama wataachana.

page

Akizungumza na kipindi cha XXL, Mabeste alisema hata akiachana na mpenzi wake Lisa ataendelea kubaki na tattoo hiyo kama kumbukumbu kwenye maisha yake.

“Hata kama let say mfano tumeachana, nitakuja kuanzisha maisha mengine na mke mwingine, yeye ataendelea kuwepo kwenye maisha yangu,” alisema. “Tayari tupo na mtoto na ndio ni kitu ambacho kitatuunganisha.

Kwahiyo yeye ni part ya maisha yangu. Ndio maana nikamchora sio kuna siku moja nitamsahau. Mimi nimechora kwa ridhaa yangu na yeye kachora kwa ridhaa yake na yote tumefanya kwa sababu ya maumivu tuliyopitia kwenye maisha yangu,” aliongeza Mabeste.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents