Burudani

Madee anena kufanya video ya katuni, ‘ni gharama kuliko video ya kawaida’

Ukitazama video mpya ya Madee ‘Sikila’ aliyomshirikisha Tekno kutoka Nigeria, utaona utofauti kwani imefanyika kwa mfumo wa katuni (animation).

Madee amesema alifanya hivyo ili kuleta utofauti katika muziki wake na aliyefanya kazi hiyo ni kijana kutoka hapa Tanzania, hata hivyo ameeleza kuwa aina hiyo ya video ni gharama zaidi.

“Kitu ambacho kimenishangaza zaidi hiyo ndiyo mara yake ya kwanza wakati nampa hiyo idea akasema siwezi, sasa mimi nilimuona wapi? alitengeneza animation moja ya Diamond na Zari kwenye tangazo fulani akamtumia Babu Tale, sasa mimi niliiona nikwambia Tale huyu jamaa ana kitu cha kufanya tumuite tumuelekeze tunataka tufanye hivyo, tukamuita tukafanya, hadi unaona hiyo video imekamilika ni miezi mitatu,” Madee ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Hiki kitu ina gharama kuliko hata video ya kawaida kuna mmoja nilimfuata muhindi aliniambia kila sekunde moja laki nikapiga hesabu nikaona ni milioni kama 16, nikaona siwezi kufanya nikarudi nikakaa na mchizi nikamuelewesha akanipa bajeti ya kawaida,” amesema.

Ameongeza kuwa licha ya kuoneka sura ya Jacqueline Wolper katika video hiyo hapakuwa na mazungumzo kati yao bali walimuweka tu.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents