Burudani

Madee: Hakuna kinachouma kama kuona wasanii wenzio wanapiga hela wakati wewe hupati kitu

Madee amekiri kuwa hakuna kitu kilimuumiza kwenye muziki kama kuona wasanii wenzake wakiwa kwenye mzunguko wa muziki wa pesa huku yeye akiwa kama mtazamaji.

madee

Akizungumza kwenye kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio jana, Madee wamewataka wasanii kuwa wavumilivu kwani hicho ndio kipindi kinachoumiza sana.

“Kwanza niwakumbushe hii ilikuwa inauma sana, mtu huwezi ukasubiri tu bila maumivu, ilikuwa inauma,” alisema. “Kwa sababu upo na watu halafu hao watu labda wewe ndo umewasogeza kwenye hiyo sehemu halafu wao wanafanikiwa halafu wewe haufanikiwi, sasa pale ukipaniki ina maana ndo unaharibu kila kitu. Kwahiyo nilichokishinda mimi ni subira. Mimi nilikuwa nasubiri lakini nilikuwa sijui nasubiria nini, lakini nilisubiri japo paniki zilikuwepo lakini nilikuwa najaribu kuzipuuza.”

“Kwahiyo kikubwa wadogo zangu ninachotaka kuwaambia ni time. Ukiona wewe unajua kabisa bado unaona ukifanya hakitokei basi ujue time bado. Time ikifika hakuna mtu ambaye anaweza kuzuia na mwenyezi Mungu anapofungua basi milango yote inafunguka kwa kitu chochote kile. Kwahiyo ukiona unafanya kitu kizuri halafu unasononeka ‘ngoma yangu haipigwi pale, ngoma yangu sijui fulani haipigi’ ujue time yako bado. Inaweza ikachezwa na watu wasiisikilize vile vile wakaiacha. Kwahiyo subira tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents