Habari

Mageuzi ya Elimu Tanzania yatikisa mkutano wa elimu duniani

Na WyEST
London Uingereza

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewasilisha Mada juu ya mageuzi ya Elimu Tanzania na kuwakosh wajumbe wa Mkutano wa Elimu Duniani unaofanyika London Uingereza.

Tanzania inashiriki katika Mkutano huo ulioleta pamoja nchi zaidi ya 200 Duniani kujadili maendeleo ya Elimu Duniani ikiwa ni nguzo kuu ya kuandaa Rasilimali watu wenye ujuzi ma mtaji mkubwa katika kuleta maendeleo.

Katika Wasilisho Prof. Mkenda ameelezea namna Tanzania ilivyoanza kazi ya utekelezaji mageuzi kwa kufanya mitaala kulenga elimu ujuzi na kusisitiza umuhimu wa wadau wa elimu wakajielekeza katika kutatua changamoto kimfumo ikiwemo ugharamiaji, vifaa, walimu bora na ujuzi.

Baada ya wasilisho hilo Mkenda pia ameshiriki katika Jukwaa la elimu kama mmoja wa wachangiaji kuhusu nini kifanyike kuwianisha Elimu jumla na amali ili kuandaa wahitimu wataokidhi mazingira ya ajira na maisha ya kazi kwa ujumla.

written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents