Habari

Makamanda India na China warudi mezani kujadili mgogoro wa mpaka

Makamanda wa India na China wamefanya mazungumzo kwa siku ya pili hii leo kufuatia mzozo mpya kuhusiana na eneo la mpaka linalozozaniwa katika jimbo la Ladakh.

Sino-Indian relations 70 years on: decoupling is not the solution - CGTN

Mataifa hayo makubwa ya Asia yamekuwa yakitupiana lawama za uchokozi mpya ikiwa ni pamoja na madai ya wanajeshi kuvuka na kuingia kwenye eneo la mwingine miezi kadhaa baada ya mvutano mbaya kabisa ambao haujashuhudiwa kwa muongo mzima.

Taarifa ya kina kuhusu mazungumzo hayo yaliyorejea asubuhi ya leo haikutolewa mara moja. Mataifa hayo mawili yameweka idadi kubwa ya wanajeshi na vifaa kwenye ukanda huo katika miezi ya karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents