Habari

Makamba akanusha uwepo wa Noti ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikil, January Makamba amekanusha taarifa zilizotolewa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kuanzishwa kwa Noti ya Pamoja ya Afrika Mashariki.

Makamba kupitia taarifa aliyoitoa katika ukurasa wake wa X amesema taarifa hizo si za kweli na mapendekezo yaliyopo hatua hiyo itafikiwa mwaka 2031.

“Hizi taarifa si za kweli, taratibu na vigezo vya kiuchumi na kitaasisi vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union)/Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika Mapendekezo ni kufika hatua hiyo mwaka 2031.” Ameandika Makamba.

Uvumi huu umeendea kupitia mtandao wa X kutoka katika ukurasa unaoitwa “Government of East Africa”.

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents