Burudani

Malumbano kati ya mashabiki wa Alikiba na Diamond yanaathiri muziki wangu – Abdul Kiba

Mdogo wake na Alikiba, Abdul Kiba amesema muziki wake unaathiriwa na malumbano yasiyoisha kati ya mashabiki wa Kiba na Diamond.

12120284_547285642095436_1812220108_n

Abdul Kiba aliyewahi kutamba na wimbo Kidela aliomshirikisha kaka yake huyo, amekiambia kipindi cha Siz Kitaa kinachorushwa na Clouds TV kuwa mashabiki wa wasanii hao wamekuwa wakimshambulia yeye bila sababu yoyote.

“Zimeathiri kwa sababu muziki umekuwa mkubwa na mashabiki wamekuwa wengi,” alisema. “Napata tabu kwa sababu naweza kupost watu wakaanza kutukana kwa sababu ya Alikiba. Maneno yanakuwa mengi lakini kwa kuwa muziki ili uweze kukua lazima ukutane na changamoto nyingi, nashukuru Mungu nimepambana nazo bado nasonga mbele,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents