Michezo

Mamadou Gaye awapa Onyo kali Mamelodi kwa Yanga

Mwandishi maarufu wa Habari za Michezo barani Afrika Mamadou Gaye amezungumza na Pitchside Podcast ya Mamelodi Sundowns kuelekea mchezo dhidi ya Yanga ametoa tahadhari kwa Mamelodi juu ya Yanga. Mamadou ametaja baadhi ya sababu zinazoipa mechi hiyo Ugumu,

Yanga kutoka kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya Azam FC hii itawaongezea umakini lakini pia kucheza fainali ya CAFCCL Msimu uliopita kunawapa shauku ya kufanya vizuri kwenye CAFCL, “Kama wameweza kucheza fainali ya CAF Confederation kwanini washindwe kucheza Nusu fainali ya CAFCL?
Kama Mamelodi Sundwons itajisahau basi nina imani itashangazwa” alisema Mamadou Gaye.
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents