Burudani

Mambo ambayo mjasiriamali anatakiwa kuyajua kuhusu kutangaza biashara yake mtandaoni

Wajasiriamali wengi wanatumia muda mwingi namna gani ya kukuza baishara zao. Kuitangaza biashara ni jambo la msingi katika kufanikiwa kibiashara na kutangaza kwenye mitandao ni muhimu zaidi hasa kipindi hiki cha sayansi na teknolojia inayokuwa kila siku.

concepts of online advertising, with message on keyboard.

Kila mjasiriamali katika nchi hii anatakiwa kujua mambo haya ili kuongeza soko lake la bidhaa anayoiuza;

  1. Uza kwa wateja ambao hawatakuacha wakati huo huo unatengeneza faida

Kwa kawaida matangazo ya biashara kwenye mitandao yanategemea uuze bidhaa kwa faida. Kitu kimoja cha msingi kujua ni kwamba kuuza inamaanisha kupata faida, lakini kuongezeka kwa gharama za matangazo yanasababisha kutopata faida iliyokuwa ikitegemewa. Kama mjasiriamali ukiweza kuwakamata wateja wako wa sasa wakawa watiifu kwako, namaanisha kwamba wauzie bidhaa madhubuti kiasi kwamba wasipate sababu ya kwenda sehemu nyingine tena. Siri iko hivi ni rahisi kumuuzia mtu ambaye ulishawahi kumuuzia kuliko kupata mteja mpya.

  1. Unatakiwa kujua watu wanafanya nini na wanapendelea kitu gani

Unapokuwa kwenye mitandao kuna habari nyingi sana za watu wanatafuta nini au wanataka kununua nini. Hivyo wanaotangaza kwenye mitandao ya intaneti wana habari nyingi kuhusu wateja watarajiwa. Kama mjasiriamali kabla ya kuanza kutangaza kwenye mtandao wowote tafuta mtandao ambao utakupa watu wanaohitaji bidhaa yako. Kumbuka usitangaze tangaze ovyo ovyo bila malengo. Kuna mifano mingi ya mitandao hiyo, mfano google kila mtu anayetumia mtandao huo kutafuta habari au kutafuta kitu cha kununua. Google wanatunza habari hizo, hivyo wanapopokea matangazo wanawalenga wale wale waliokuwa wakitafuta kitu kama hicho, vivyo hivyo Facebook hutafuta watu wanaoelekeana kwa namna ya habari wanazozifuatilia kwa ukaribu.

3. Mitandao ya kijamii ni mizuri kwa wewe kujitangaza

Wafanya biashara wengi wadogo wadogo wanaogopa sana mitandao ya kijamii. Ingawa inaweza isiwe mizuri sana katika matangazo lakini inakupa uhuru wa kuwafikia watu ambao huwezi kuwafikia kirahisi. Jaribu linked in kama unatangaza kwa makampuni na Facebook kama unatangaza kwa watumiaji wa mwisho ingawa biashara nyingi zimeendelea kunufaika na matangazo ya Facebook. Jaribu Twitter Video ads, Stumble upon’s Paid Discovery, Google+ na mingine mingi kuwafikia walengwa wako.

  1. Kujaribu hakuwezi kukupa faida ya haraka

Wakati unajaribu njia nyingine ya kutangaza biashara yako haiwezi kukupa faida papo hapo haimaanishi uachane na hiyo njia mpya. Unahitaji kupata njia mpya ya kujitangaza ili ujulikane zaidi, hivyo ongeza watu wengi zaidi wanaokutana na biashara yako mara kwa mara kwenye mitandao.

  1. Ongeza matangazo yako kadri unavyojifunza.

Unapotumia Google Analytics inakupa taarifa kitu gani kinaendelea kwenye blogu yako au tovuti yako n.k. Mfano wa mtandao huo utajua ni watu wa aina gani hupendelea kufuatilia bidhaa zako na ni wa umri gani na wewe unachukua hatua gani kujitangaza zaidi? Mfano mwingine facebook vile vile inakuonyesha rika la watu wanaofuatilia ukurasa wako wa bidhaa. Maamuzi yanabaki kwako unaongeza matangazo wapi na kwenye mtandao gani ili uweze kuuza zaidi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents