Habari

Maoni ya Zitto juu ya katazo la Rais Magufuli kuhusu kusafirisha mchanga

Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo ametoa maoni yake juu ya katazo la Rais Magufuli kutotaka mchanga usafirishwe nje ya nchi huku akidai Raia mwema wameuliza maoni yake juu ya zuio hilo.

Zitto ametoa maoni yake haya kupitia mtandao wake wa kijamii:

RaiaMwema waliniuliza maoni yangu kuhusu zuio la kupeleka nje mchanga wa madini. Haya Ndio majibu yangu ambayo yamenukuliwa na Toleo la Leo la gazeti Hilo, Toleo namba 500 la 8/3/2017.

“Kuweka zuio la kusafirisha mchanga wa dhahabu ni uamuzi sahihi uliofanywa bila kuzingatia kwanza uwezo wa ndani wa kuchenjua ( refinery).

Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini, haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa ( economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 Hivi. Pia tunahitaji umeme zaidi ya 1500MW kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama potential ya hii region ya kuzalisha Hizo copper concentrates ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye region.

Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo. Sasa mjadala hapa ni kwanini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio alilotoa Rais Ndio litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi Sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili Kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa. Kwahiyo AMRI ya Rais iwe ni kuleta mjadala kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana.

Lakini pia wataalamu wanaweza kukaa na kubuni teknolojia yenye uwezo wa kufanya uchenjuaji kwa kiwango cha mchanga tunachozalisha nchini. Haiwezekani dunia nzima ikawa na teknolojia moja tu ya tani 150,000 la hasha.

Ushauri wangu ni kwamba Serikali ikae na sekta ya madini ili kupata jawabu la kudumu na kuweka commitment ya muda maalumu kuendelea kusafirisha mchanga na baada ya muda huo mchanga huo uchenjuliwe nchini kwetu na kuzalisha ajira na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha. Hii sio Zero-Sum game ( Kama sio kusafirisha basi hakuna lingine). Hapana. Mjadala unaweza kuleta jawabu lenye faida kwa nchi”

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents