Burudani

‘Maproducer wengi ni Feki’ – Sheddy Clever

Muaandaji wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Sheddy Clever amewachana Maproducer wenzake kwa kusema kuwa wengi wao ni Feki.

Tokeo la picha la sheddy clever
Mtayarishaji wa muziki ‘Sheddy Clever’

Mmiliki huyo wa Studio za Burn Records amesema kwa sasa muziki wetu ulipofikia ni sehemu ambayo Maproducer wengi wanaunga unga tuu Midundo tofauti na wale wazamani walivyokuwa wanagonga Beats, hivyo ameiomba serikali kutunga sheria kuwatoa maproducer hao Feki.

Maproducer wengi sasa hivi ni feki yaani hamna producer real ukiangalia toka enzi zile akina P-Funk Majani ni muziki ambao unadumu na changamoto hazikuwa nyingi, hata ule msemo kuwa muziki unabebwa na video hata mimi nakubaliana nao kwani nyimbo zimekuwa mbovu sana,mimi nafikiri maproducer tujitambue na tusikubali kupelekwa ovyo ovyo na Wasanii“Amesema Sheddy Clever.

Sheddy Clever ameeenda mbali zaidi kwa kuiomba Serikali kuingilia kati suala la za haki mmiliki na kutunga Sheria ili kuwabana baadhi ya Maproducer Feki ambao wanaongezeka kila kukicha.

Ingekuwepo sheria kali kwa maproducer ambao wapo real ndiyo wafanye kazi wapewe vibali  husika vya kufanya kazi na wanatambulika kiserikali au BASATA kwahiyo kuwe na sheria ngumu iwekwe kuanzia kwenye ukaguzi wa ngoma“Amesema Sheddy Clever kwenye mahojiano yake na eNEWS ya EATV.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents