Habari

Marekani, Korea Kusini zaungana kwenye mazoezi ya kijeshi kuitishia Korea Kaskazini

Jana tarehe 3 Desemba 2017,  Jeshi la anga la Marekani na la Korea Kusini yameungana na kuanza kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja ambapo hii inakuwa ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo.

Ndege za kisasa za kijeshi aina ya F-22 Raptor stealth fighters zilizotumiwa jana na Marekani kwenye mazoezi hayo.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa jeshi la Marekani imeeleza kuwa majeshi yake yanafanya hivyo ili kujiimarisha na imepeleka ndege 230 za kivita kwenye mazoezi hayo ambayo hufanya kila mwaka.


Mazoezi hayo ambayo yanafanyika katika rasi ya Korea yametajwa kuwa ni kitisho kwa Korea Kaskazini ambayo siku wiki iliyopita ilifanya majaribio ya Lombora kubwa zaidi la nyuklia ambalo ilithibitisha kuwa linauwezo wa kuipiga Marekani na Uingereza sehemu yoyote ile.

Soma zaidi-Korea Kaskazini yafanya jaribio lingine la kombora, Yadai sasa inaweza kuipiga Marekani popote

Jeshi la Marekani limeeleza kuwa kuwa zoezi hilo la pamoja ni la kuhakikisha kuwepo amani na usalama katika rasi ya Korea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents