Habari

Marufuku kuvaa hijabu au niqab Uswisi (+ Video)

Uswizi imepiga kura ya kuunga mkono marufuku ya kuvaa hijabu katika maeneo ya umma ikiwemo burka na niqab zinazovaliwa na wanawake wa dini ya Kiislamu.

Matokeo rasmi yanaonesha kwamba waliounga mkono kura hiyo ya maoni iliyofanyika Jumapili ni asilimia 51.2 huku idadi ya waliopinga ikiwa ni asilimia 48.8.

Mswada huo uliwasilishwa na mrengo wa kulia wa chama cha Swiss People’s Party (SVP) ambacho kilifanya kampeni yake kwa kutumia misemo kama vile “Sitisha itikadi kali”.

Kundi kubwa la Kiislamu nchini Uswizi limesema kuwa hiyo ni “siku ya huzuni kubwa” kwa Waislamu.

“Uamuzi wa leo umefungua vidonda vya kale, na kuongeza pengo la ukosefu wa usawa kisheria, na ishara ya wazi ya kutengwa kwa kundi la Waislamu waliowachache,” Baraza la Waislamu nchini humo limesema katika taarifa iliyotoa, na kuongeza kwamba huenda likapinga uamuzi huo mahakamani.

Serikali ya Uswizi ilikuwa imejitetea dhidi ya marufuku hiyo kwamba siyo jukumu la serikali kuamua kile watakachovaa wanawake.

Kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Lucerne nchini Ujerumani, ni sawa na kusema hakuna anayevaa burka na ni wanawake takriban 30 tu wanovaa niqab. Karibu asilimia 5 ya idadi ya watu nchini Uswizi ambayo ni milioni 8.6 ni Waislamu, wengi wao wakiwa wanatoka chuo kikuu cha Uturuki, Bosnia na Kosovo.

Watu nchini Uswizi wana uhuru katika masuala yao binafsi chini ya mfumo wa nchi hiyo unaozingatia demokrasia.

Na mara nyingi huwa kunafanyika kura za maoni juu ya masuala mbalimbali ya kitaifa au eneo.

Hii sio mara ya kwanza suala linalohusu Uislamu kufanyiwa kura ya maoni nchini Uswizi.

Mwaka 2009, raia walipinga ushauri wa serikali na kupiga kura ya maoni inayounga mkono kupiga marufuku majengo yenye minara kama misikiti – hoja iliyowasilishwa na chama hicho hicho cha SVP na kusema kuwa minara ni ishara ya Uislamu.

Wanawake wakiwa wamevalia vazi la Niqab
 

Mswada huo iliopigiwa kura ya maoni Jumapili haukutaja Uislamu moja kwa moja na pia ulilenga kusitisha wanaondamana katika maandamano ya ghasia wakiwa wamevaa barakoa zinazowaziba uso.

Hata hivyo, marufuku hiyo ilikuwa inafahamika sana kama “upigaji marufuku burka”.

Sanija Ameti, mwanachana wa chama cha Waislamu Uswizi, ameliambia shirika la BBC kuwa kampeni hiyo – na kuoneshwa kwa michoro ya wanawake Waislamu katika mabango imekuwa hatua ya kukasirisha.

“Waislamu wengi nchini Switzerland watahisi kutukanwa na wasio sehemu ya jamii hii na kujisukuma katika sehemu wasiostahili. Sisi hatufanani na michoro ya wanawake kwenye mabango, hapana,” alisema.

Hata hivyo, wengine katika jamii ya Kiislamu wameunga mkono marufuku hiyo.

Imam Mustafa Memeti, kattika mji wa Bern, ameliambia shirika la BBC kwamba mtazamo wake, kampeni hiyo ilikuwa “inapinga Usilamu”. Lakini alisema kwamba aliunga mkono hoja hiyo kwasababu ingesaidia kuleta uhuru kwa wanawake wa Switzerland.

Kabla ya kura hiyo ya maoni, Walter Wobmann, mwenyekiti wa kamati ya kura ya maoni na mbunge wa chama cha SVP, ameelezea hatua ya Waislamu kufunika uso kama “ishara ya itikadi kali, siasa zinazoegemea Uislamu ambazo zimekuwa zikiongezeka barani Ulaya lakini zisizo na nafasi nchini Uswizi”.

“Nchini Uswizi utamaduni wetu ni kwambza unaonesha usoa wako. Hii ni ishara ya uhuru wetu wa msingi,” amesema.

Wanawake Waislamu
Shirika la Amnesty International limezungumza dhidi ya mafuruku hiyo, na kuitaja kama “sera hatari inayokiuka haki za wanawake ikiwemo uhuru wa kujieleza na wa kidini”.

Uvaaji wa hijabu au kijistiri kichwa na kufinika uso kwa Waislamu katika maeneo ya umma kumeleta mjadala mkali katika nchi zingine za Ulaya.

Ufaransa ilipiga marufuku uvaaji wa hijabu inayofunika uso wote mbele ya umma mwaka 2011 huku Netherlands, Denmark, Austria na Bulgaria zikiweka marufuku ya kudumu au ya muda ya kufunika kabisa uso unapokuwa maeneo ya umma.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CMJf-Ghh7ka/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents