Burudani

Matonya adai ana hofu na hili la serikali kuhamia Dodoma

Wakati serikali ya Magufuli ikiendelea kukamilisha mpango wake wa kuhamia Dodoma, msanii mkongwe wa muziki, Matonya amedai yeye ni mmoja kati ya watu ambao hawajui kwanini serikali imeamua kuhamida Dodoma.
12224097_927597553975092_1780800703_n

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Matonya amesema serikali ilitakiwa kutoa elimu yakutosha kwa wananchi kuhusu suala la serikali kuhamia Dodoma.

“Kusema kweli mimi sifuatilii haya mambo, lakini kwenye hili la kwenda Dodoma kama silielewi elewi hivi. Yaani serikali haikutoa elimu yakutosha juu serikali kuhamida Dodoma maana yake ni nini, kwa sababu kuna watu wengi kama mimi sijui maana yake ingawa najua Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania,” alisema Matonya.

Pia muimbaji huyo alisema hizo gharama ambazo zinatumika kuijenga Dodoma ni bora zingetumika katika shughuli nyingine za kimaendeleo.

“Mimi naona kama kuna pesa nyingi zinaenda kutumika kwa ajili ya kuandaa miundombinu, unajua mji wa Dar es salaam tayari ulishajiseti, labda tuangalie itakuwaje lakini kusema kweli mimi ni mmoja ya raia wa kawaida ambao bado sijajua nini maana ya serikali kuhamia Dodoma,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents