Habari

Mbowe ampinga Rais Magufuli kuhusu wawekezaji kunyang’anywa viwanda

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA), Mhe Freeman Mbowe amesema Serikali haiwezi kujenga viwanda peke yake bila kuihusisha sekta binafsi ambayo ndiyo mdau mkuu katika sekta ya uwekezaji nchini.

Mbowe amepinga kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John P. Magufuli ya kuwanyang’anya wawekezaji waliobinafsishiwa viwanda na kushindwa kuviendeleza kwa kudai kwamba serikali ilitakiwa kutafuta chanzo cha kufungwa kwa viwanda hivyo kabla ya kufikia uamuzi huo.

“Hakuna mfanyabiashara duniani àmbaye atapewa kitega uchumi kinachozalisha halafu akakifunga, Hayupo”,amesema Mhe Mbowe leo Julai 31 kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Rais Magufuli aagiza waliobinafsishiwa viwanda kuvirejesha serikali

Akitaja sababu za  mbalimbali zilizofanya viwanda hivyo visifanye kazi, Mhe Mbowe amesema kuwa ni pamoja na kutopatiwa ruzuku kutoka Serikalini na mfumo hodhi wa soko uliokuwepo kipindi viwanda hivyo vinajengwa.

Hata hivyo, Mbowe amesema Rais Magufuli hana mapenzi na sekta binafsi kwa kuwa anaamini kwamba kila mtu aliye kwenye sekta binafsi ni mpiga dili.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents