Habari

Mbunge Ester Bulaya asema hatorudi nyuma kwenye vita dhidi ya ‘Wazee wa Unga’

Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara, Ester Amos Bulaya amesema ataendeleza vita dhidi ya mtandao wa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya nchini licha ya kupokea vitisho kuwa anaweza kuuawa.

bulaya

Mbunge huyo alitoa hoja bungeni kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia wahalifu wa dawa za kulevya.

Akizungumza Clouds FM jana kwenye kipindi cha Amplifaya alisema baada ya kuwalikisha hoja hiyo alipokea zaidi ya jumbe 2,000.

“Nimepata maoni mbalimbali ya kwenye mitandao,simu nimetumiwa meseji za kufurahisha na kunitia moyo. Lakini kuna baadhi ya wachache ambao wanakuwa na hofu kuniambia ‘watakuua, watakutaka kucha’ something like that. Lakini nilicho waambia hatuwezi kuacha kusema vitu vya msingi ambavyo vinagusa taifa letu,vinachafua taifa letu katika anga za kimataifa.Lakini hatuwezi kuacha kuzungumzia mtandao wa madawa ya kulevya eti kwasababu wanaoneka ni untouchable ni watu wenye fedha,” alisema.

“Naamini mheshimiwa Amina Chifupa ametangulia mbele ya haki lakini lazima alichokianza wengine wakiendeleze kwasababu inaonekana alikuwa ana dhamira njema na yeye mbali ya kuchangia na mimi lazima nipeleke hoja bungeni nionyeshe tatizo liko wapi na lazima watu wataje, na wasiwe miungu watu, na hatua zichukuliwe kukomesha biashara haramu ya madawa ya kulevya. Siogopi na wala sitoogopa na naamini kama ikitokea Ester Nimepigwa au nimekufa hakuna binadamu anayeweza kumuua binadamu mwenzake. naamini siku yangu itafika au Mungu ameamua kuchukua roho yangu kupitia wao. Kwahiyo wasije wakaona wao mashujaa kwa kutoa roho ya Ester kwamba kwakuona vita hii haitaendelea. Watakuepo akina Ester wengi ambao wanapinga madawa ya kulevya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents