Habari

Mbunge wa CCM amtolea uvivu Mhe Kigwangalla ‘unakuwa sehemu ya wachochezi’

Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe Ridhiwani Kikwete amemjibu kwa kumshangaa, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Dkt Khamis Kigwangala aliyeuliza je, kuna tatizo la ajira au watu wanachagua kazi? kwa  kumwambia anaweza kuwa sehemu ya wachochezi kwa swali lake.

Mbunge wa jimbo la Chalinze, Mhe Ridhiwani Kikwete

Mhe Ridhiwani Kikwete amemjibu Mhe Kigwangalla kwa kumwambia kuwa huenda kauli yake ya kuhoji uwepo wa ukubwa wa tatizo la ajira nchini Tanzania na uchaguaji wa kazi ikawa chanzo cha uchochezi, licha Mhe Kingwangalla kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma cha kuwafanyia usaili maelfu ya wataalamu waliojitokeza kwenye usaili  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao umefanyika jana alhamisi Agosti 30, 2017.

Je, hii inaashiria ukubwa wa tatizo la ajira nchini ama ni kwamba watu wetu wanachagua sana kazi za kwenda?“ameandika Mh Kingwalla kwenye ukurasa wake wa Twitter na ndipo Mbunge wa jimbo la Chalinze akamjibu kwa kumwambia ” Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakuwa sehemu ya wachochezi! Mh. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lkn picha inatoa jibu sahihi.”

SOMA ZAIDI- Zaidi ya watu elfu 30 kufanya usaili wa nafasi 400 TRA

Hata hivyo, swali hilo la Mhe Kigwangalla halikumgusa tu Mhe Ridhiwani Kikwete bali liliibua pia maswali mengine kwa Watanzania ambao wanamfuata Mhe Kigwangalla kwenye mitandao ya kijamii,  wengi wakihoji kuwa mpaka sasa Kigwangalla bado hajui ukumbwa wa tatizo la ajira kwa vijana nchini Tanzania?.

Majadiliano hayo mazito kuhusu ajira yameibuka mitandaoni kuanzia jana baada ya kujitokeza zaidi ya watu elfu 56,000 waliojitokeza kuomba nafasi 400 za ajira zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents