Habari

Mchungaji Nigel Gaisie wa Ghana aahidi kumfufua Kobe Bryant na mwanae GiGi ila apewe asilimia 10 ya utajiri wake

Mchungaji Nigel Gaisie wa Ghana aahidi kumfufua Kobe Bryant na mwanae GiGi ila apewe asilimia 10 ya utajiri wake

Mchungaji Nigel Gaisie wa nchini Ghana amesema anaweza kumfufua nyota wa kikapu wa Marekani KobeBryant pamoja na mwanae Gianna endapo atapewa alimia 10 ya utajiri wa mchezaji huyo Kobe, mwanae na watu wengine 7 walifariki katika ajali ya helikopta mjini Los Angeles, Januari 26.

Habari hii itatikisa ulimwengu wote kwa sababu ya jinsi mtu huyu ni mkubwa. Ninaona watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wakizungumza juu ya mtu huyo kwa wiki kadhaa zijazo ninaona sura nyingi za kusikitisha. ” “Taifa la Marekani litamuomboleza huyu mtu mkuu. Bwana aliniamuru nitangaze kwa familia ya mtu huyu, balozi kuwa Bwana hakuamua kifo cha mtu huyu.

Akaniambia tena, ‘Nigel, uwaambie familia ya mtu huyu na uwaambie ulimwengu wote, ikiwa watakubali kutoa sadaka nitakutumia kama chombo kumfufua mtu huyu na binti yake.’ ” Nabii Nigel alisema kuwa bila ofa hiyo ya 10%, ya mali zake  hakuna kinachoweza kufanyika ikiwa ni kufufua mchezaji huyu aliyestaafu wa NBA.

“Mtu huyo ana thamani ya dola milioni 500 na ikiwa familia itakubaliana kunipa 10% ya mapato yake, nitawarudisha mtu wao kwenye maisha ya kawaida.

Bwana asema hivi. Bila pesa, siwezi kumrudisha yeye na yule msichana mdogo amabye ndio binti yake ”alisema.

Mtumishi huyo wa Mungu  aliwasihi watu kwenye mkutano huo kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wa karibu na familia ya marehemu Kobe Bryant. Mwishowe, aliwaonya washirika wake wasiwe na shaka maneno ya Mwenyezi Mungu au la sivyo watakabiliwa na athari kubwa.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents