Michezo

Messi awa mchezaji anaelindwa zaidi Duniani (Video)

Wengi tunafahamu kuwa Messi analindwa na mlinzi wake maarufu Yassine Chueko, Huyu Mwamba ni Mwanajeshi mstaatu, pendekezo la ajira ya Chueko ilikuwa ni pendekezo kutoka David Beckham. Inaelezwa Chueko haifanyi kazi peke yake, nyuma yake kuna walinzi wengi ambao hutazama usalama wa Bwana Mkubwa Messi ndani na nje ya Uwanja.

Chueko anaongoza timu ya wanausalama zaidi ya 50 ambao wanafanya kazi bila kuchoka kuhakikisha usalama wa Messi, wengine huwa majukwaani na wengine huwa karibu na uwanja, wapo baadhi hukaa nje kutazama hali ya usalama ila mara nyingi Chueko ndo anashughulikia usalama karibu na Messi. Hata akienda kushangilia basi Chueko anasogea karibu ili tu kuhakikisha kwamba Boss haguswi na watu wasiohusika.

Kwa siku za karibu Chueko ameongeza walinzi wengine sio chini ya 10 kumsaidia ulinzi wa ndani ya uwanja huku wengine wakiendelea nje ya Uwanja.

Chueko kabla ya kustaafu Jeshi aliwahi kwenda Iraq pamoja na Afghanistan kama Mwanajeshi wa Marekani (Navy Seal) na uwezo pamoja na utaalamu wake katika usalama unazidi kumuongezea umaarufu mkubwa kwani kazi zake anafanya kwa weredi mkubwa sana.

Kwa sasa ni ngumu shabiki kumgusa Messi kwa sababu walinzi wameongezeka, wamekaka kila pembe ya Uwanja kuhakikisha usalama wa Messi.

Unahisi kwanini Messi analindwa zaidi hivi??

Kuangalia video kamili bonyeza Link hapa chini:

https://www.instagram.com/reel/C6F_FACNMB7/?utm_source=ig_web_button_share_sheet

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents