Burudani

Mfahamu K.O, rapper wa South aliyeshirikishwa na Vanessa Mdee kwenye ngoma yake mpya ‘Nobody But Me’

Wiki Ijayo, Vanessa Mdee ataachia ngoma yake ya kwanza aliyomshirikisha msanii nje ya Tanzania.

11055963_710795605704851_1443752919_n

Kwenye ngoma hiyo ‘Nobody But Me’ itakayotoka na video yake, Vanessa amemshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O.

Rapper K.O. was born Ntokozo Mdluli

K.O ni nani?

K.O ni rapper maarufu na anayekubalika nchini humo ambaye level zake ni sawa na AKA na Cassper Nyovest. Rapper huyo alizaliwa kwa jina la Ntokozo Mdluli huko Soweto, Johannesburg kwa wazazi wake Thembisile Mdluli na Jabulani Mdluli.

Akiwa bado mtoto mchanga, familia yake ilihamia kwenda Piet Retief huko Mpumalanga ambako alikulia. Wasanii waliomvutia K.O kufanya muziki ni pamoja na Snoop Dogg na Dr Dre na walikuwa wasanii ambao walimfanya naye atake kuwa MC na kuota kuwa siku moja naye atakuja kuwa nguli kwenye Hip Hop na hivyo safari yake ikaanza.

Pindi K.O ameanza kufanya muziki kama kazi alikuja kukutana na Ntukza a Ma-E kwenye chuo kikuu ha teknolojia cha Vaal ambako alipata shahada ya mahusiano ya jamii.

bet-teargas
Teargas

Watatu hao walianzisha kundi lao walilolipa jina la Teargas ambalo hadi leo limeshatoa album zilizoshinda tuzo na kukubalika ‘K’shubile K’bovu’, ‘Wafa Wafa’, ‘Dark Or Blue’ na ‘Num8er Num8er’.

Mafanikio na umaarufu wa kundi la Teargas yalimsaidia K.O kujitengeneza kuwa staa anayejitegemea na kwa kupitia collabo anazofanya, zimemfanya kuwa member maarufu zaidi wa kundi hilo.
Miongoni mwa collabo alizowahi kufanya ni pamoja na ‘God’s Will’ akiwa na AKA, ‘We Rolling’ akiwa na L-Tido na ‘Just Dream’ ukiwa ni wimbo wa kampeni ya Hansa Pilsener akiwa pamoja na Zakes Bantwini msanii wa Big Nuz, Mampintsha.

Mwaka 2013, K.O pamoja msanii mwenzie wa kundi la Teargas, Ma-E walijiunga na mkongwe wa masuala ya muziki na masoko Thabiso Khati kuanzisha label ya Cashtime Life.

10727362_349849081891444_218632015_n
Vanessa Mdee na K.O

K.O akawa msanii wa kwanza wa kampuni hiyo kwa kutoa single yake ‘Mission Statement’ iliyofanya vizuri.

March 3 mwaka jana, K.O aliachia single yake ya pili ‘Caracara’ aliyomshirikisha msanii mwingine wa Cashtime Life, Kid X.

Caracara ikaja kuwa single maarufu zaidi nchini humo kwa kutawala mawimbi ya redio na mauzo ya mtandaoni. Ngoma hiyo ilikamata nafasi ya kwanza kwenye chart za MTV, Trace TV, Channel O, Metro FM, YFM, 5 FM, Ukhozi FM na stesheni zingine barani Afrika.

Album ya kwanza ya K.O iliingia sokoni tarehe 27 October 2014.

August mwaka jana K.O na AKA walikuja kukutana tena kwenye ngoma nyingine. Ni Run Jozi iliyopo kwenye album ya AKA, Levels. Ngoma hiyo ilifanikiwa mno kwa kushika chart karibu zote maarufu.

Kwahiyo Vanessa Mdee amefanikiwa kumweka mtu mwenye nguvu mno barani Afrika na anayechukuliwa kuwa miongoni mwa waandishi hatari zaidi wa mashairi si nchini Afrika Kusini peke yake.

10914624_1401963063452415_1631775270_n

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents