Habari

Mfanyabiashara aliyemuua mkewe na kumchoma moto, aiomba mahakama impatie fedha zake

Mfanyabiashara aliyemuua mkewe na kumchoma moto, aiomba mahakama impatie fedha zake

Mfanyabiashara Hamis Said(38), anayekabiliwa na kesi ya mauaji, ameiomba Mahakama apatiwe fedha zake zaidi ya Shilingi Milioni 5.


Ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa fedha hizo zipo kwenye laini zake mbili za simu ya mkononi(Airtel na Tigo) na anahitaji ili zimsaidie kwa matumizi yake na familia ikiwemo kumlipia mwanaye karo ya shule.
Baada ya kuwasilisha ombi hilo Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amesema kuwa hawawezi kumpatia laini hizo kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea.
Bwana Said anatuhumiwa kumuua Mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuteketeza mwili kwa magunia mawili ya mkaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents