Burudani

Michelle Obama: ‘Nataka kuwa kama Beyonce’

First Lady wa Marekani Michelle Obama amesema kama asingekuwa hapo alipo sasa angetamani kuwa kama Beyonce.
Michelle na Beyonce wameanzisha urafiki wa karibu miaka ya hivi karibuni tangu mwanamuziki huyo ambaye ni mke wa Jay-Z atumbuize mbele ya rais Barack Obama mwaka 2009.
Na sasa uhusiano wao umeingia hatua mpya kutokana na Michelle kuweka wazi kuwa anatamani kuwa mwimbaji kama Beyonce.
“Inaonekana wanamuziki hufurahia sana kazi yao,” Michelle ameliambia jarida la People.

Mwezi uliopita Beyonce aliandika barua ya mkono kwa Michelle na kumwambia kuwa angependa Michelle awe role model kwa mwanae Blue Ivy.
Katika barua hiyo Beyonce aliandika “Michelle, ni mfano halisi wa mwanamke shupavu mmarekani mwenye asili ya Afrika. Ni mama mwenye kujali, mke mwenye mapenzi ya dhati wakati huo huo ni FIRST LADY!!!! Pamoja na pressure, na stress za kumulikwa na darubini- ni mnyenyekevu, mwenye mapenzi na mkweli.
Huijenga na kuilea familia yake wakati huo pia akiwaangalia mamilioni wengine kwa namna nyingi. Michelle, asante sana kwa kila jambo unalolifanya kwetu – Najivunia kuwa na mwanangu anayekua katika ulimwengu ambao ana watu wa kuwaangalia. Love, Beyonce.” (Beyonce)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents