Habari

Mimi nimefukuzwa tena kwa aibu na kutukanwa – Bernard Membe

Aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bernard Kamilius Membe hii leo Julai 16 ametangazwa rasmi kujiunga na na ACT Wazalendo yeye na familia yake.

Bernard Membe aeleza tofauti ya 'CCM ya zamani na CCM mpya' - BBC ...

Baada ya kutangazwa Membe amesema kuwa “Kuna watu wameniuliza wewe hautakuwa kama yule wa kwenda na kurudi nyumbani, hapa mimi ndiyo nyumbani kwangu, mimi ni mbele kwa mbele, mazingira yaliyonifanya mimi niingie ACT ni tofauti kabisa yaliyomfanya mwenzangu akaenda kule na kurudi” – Bernard Membe

“Mimi nimefukuzwa tena kwa aibu na kutukanwa na vijana ambao ningeweza kuwazaa, na sikutenda kosa lolote hata mbele ya Mungu, kosa nililofanya ni la kugombea Urais 2015, milango imefungwa na kufunguliwa na ACT na nikakaribishwa chumbani” – Bernard Membe.

“Kiongozi wangu @zittokabwe wewe ni mfano wa vijana na ninashukuru vijana wadogo kama kina Nondo unawalea, toka tulipokutana miaka ya 2000 ukiwa na Mama yako mzazi, wewe unapenda binadamu na kuheshimu wenzako, Mungu na Malaika wako na wewe” – Bernard Membe.

“Kuna watu wameniuliza wewe hautakuwa kama yule wa kwenda na kurudi nyumbani, hapa mimi ndiyo nyumbani kwangu, mimi ni mbele kwa mbele, mazingira yaliyonifanya mimi niingie ACT ni tofauti kabisa yaliyomfanya mwenzangu akaenda kule na kurudi” – Bernard Membe

“Mkoa wangu wa Lindi na Mtwara hivi sasa wanasubiri kuhamia @ACTwazalendo  hivi ninavyozungumza nina wanachama wa CCM wanataka wajiunge, lakini jumla yake tuna kadi zisizopungua 8960 ambazo zitakazomiminika kwangu ili nizirudishe @ccm_tanzania – Bernard Membe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents