Habari

Mmoja akamatwa kwa kupandisha Bei ya Sukari

Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba, amefanya ziara ya kushtukiza katika oparesheni inayoendelea ya kuhakikisha Sukari inauzwa kwa bei elekezi  na kuwafichua wanaouza Sukari kwa bei Kubwa  huku mfanyabiashara mmoja akikamatwa kwa kuuza bei ya shilingi 189,000 kwa mfuko wa Sukari wenye ujazo wa Kilo 50 tofauti na bei elekezi ya Serikali.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya Barabara inayosimamiwa na wakala wa barabara za mjini TARURA, masafara huo wa Mkuu wa Mkoa ukipita katikati ya Mji wa Manyoni lilionekana gari lililobeba shehena ya Sukari, na baada ya kuulizwa walidai wamenunua kwenye duka la mfanyabiashara huyo aliyejulikana kwa jina la Mayengela Mbonji.

Baada ya maelekezo ya wateva hao Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba aliyeambatana na kamati ya Usalama Wilaya ya Manyoni, wakaingia katika duka hilo na kukagua risiti za mauzo ambapo ikabainika anauzia wateja kwa bei kati ya shilingi 184,000 hadi 189,000 kwa mfuko wenye ujazo wa Kilo 50.

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents