Habari

Mourinho awasili Ureno kwa mazishi ya baba yake mzazi (+Picha)

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho tayari ameshafika nchini Ureno kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi.

Jose Mourinho na Baba yake mzazi

Baba yake Mourinho aitwae Jose Manuel Mourinho Felix 79 amefariki Dunia wikiendi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo huko jijini Setubal nchini Ureno.

Mapema jana Mourinho kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya baba yake huku ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe (B&W) na hakuandika kitu huku maoni ya mashabiki wakionekana kumpa pole kwa msiba uliompata.

https://www.instagram.com/p/BVxoRvQAZT2/?taken-by=josemourinho

Katika enzi za uhai wake Baba mzazi wa Mourinho alishawahi kuitumikia timu ya taifa ya Ureno na Klabu ya Victoria Setubal FC kwa michezo 250.

Tazama picha za Mourinho alivyowasili Ureno kwa kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi.

Jose Mourinho is comforted by a friend following his father's passing on Sunday
Mourinho akipokelewa na baba yake mdogo mapema leo
Mourinho (2nd left) was accompanied by family including daughter Matilde (2nd right)
Mtoto wa kike wa Mourinho wa pili kulia nae alikuwepo kwenye mapokezi ya baba yake mzazi
The group attended a church service ahead of Felix's funeral on Tuesday morning
Mourinho na Binti yake wakitoka kanisani kwa misa ya marehemu baba yake .

Felix, who had been suffering from ill health for several months, died in Setubal

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents