Burudani

Mpango wa Weusi kwa miaka 10 ijayo

Msanii wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ambaye pia ni msemaji wa kundi hilo amesema mpango wao ni kutoa hit kwa miaka 10 ijayo.

Nikki wa Pili ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Quality Time’ ambayo amemshirikisha member mwenzake kutoka Weusi G Nako, ametumia ukurasa wake wa twitter kueleza hayo;

Toka 2006 mpaka 2017…….tumepiga Hits bila break……tunampango wa kufanya hivyo miaka 10 ijayo pia…..watu wabaya Weusi

Kwa mwaka huu pekee Weusi wametoa hit kama Yakulevya na Dude ingawa ngoma hizi hazina video, pia kuna hit za solo project ambapo Joh Makini ametoa nyimbo kama Waya na Kata Leta aliyomshirikisha Davido, naye G Nako ametoa ngoma ‘Lucky Me’ na Nikki ‘Quality Time’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents