Burudani

Mr Ttouch kuwarudisha Mandojo na Domokaya ?

Mtayarishaji wa muziki, Mr Ttouch amedai Mandojo na Domokaya ni wasanii ambao bado wanahitajika katika tasnia ya muziki.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Mr Ttouch amedai kila asikisikiliza nyimbo za wasanii hao bado anaona kuna vitu wanatakiwa kuvifanya katika muziki kwa sasa.

“Kusema kweli Mandojo na Domokaya ni wasanii ambao kila nikisikiliza kazi zao za zamani naona bado kuna kitu fulani hivi ambacho hakipatikani katika muziki wa siku hizi. Sina mpango wa kufanya nao kazi lakini ni wasanii ambao bado wana nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi kama wakipata nafasi kama zamani. Lakini kama ikitokea nafasi ya kufanya nao kazi nitafanya kwa sababu ni wasanii wazuri na bado nawakubali sana” alisema Mr Ttouch.

Ttouch alisema muziki wa wawili hao ulikuwa na ladha tofauti ambayo hata vijana wa leo wakipewa wanaweza kuikubali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents