Burudani

Mrisho Mpoto apata shavu la ubalozi wa kampeni ya ‘Kili Challenge’

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amepata shavu jipya la kuwa balozi wa kampeni ya ‘Kili Challenge’ itayokuwa inaelimisha jamii kuhusu kuendeleza mapambano dhidi ya Ukimwi.
Mpoto
Mpoto akisaini mkataba

Kupitia instagram, Mpoto ameandika:

Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) imeniteua kama msanii na mtanzania kuwa Balozi wa Kampeni ya Kili Challenge.
Napenda kuwashukuru sana TACAIDS na GGM kwa kuniamini na kunipa fursa hii ya kipekee.
Naomba nitoe wito kwa watanzania na waafrika wote kuwa tuendelee na mapambano dhidi ya Ukimwi. Tuzungumze na tuchukue hatua dhidi Ukimwi ili tufikie lengo la Kampeni ikiwa kama lengo letu sote tuhakikishe tunafikia idadi ya Zero katika Maambukizi Mapya, Zero ya Unyanyapaa, Zero ya vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents