BurudaniHabariLifestyle

Mtoto wa 50 Cent amjia juu baba yake, hela ya matunzo dola 6,700 mwezi ndogo

Mtoto wa kwanza wa  50 Cent Marquise Jackson mwenye umri wa miaka 25 anadai kiasi cha pesa alichopokea kila mwezi kama matunzo ya mtoto kutoka kwa babake hakikutosha.

Hivi majuzi, Marquise Jackson alienda kwenye Instagram Live na mjasiriamali na rapa wa zamani Choke No Joke na kuelezea kusikitishwa kwake na baba yake na malipo yake ya watoto.

Kulingana na maelezo yake alieleza kuwa baba yake yaani 50 Cent analipa dola 6,700 sawa na T sh milioni 15. 6 kwa mwezi hazimtoshi kumudu maisha aliyodai kuwa alihitaji katika jiji la New York.

Kama anavyoonekana kwenye video akiongea anasema kuwa:

“Unamzungumzia mtu ambaye yupo katika orodha ya Forbes, unazungumza juu ya mtu ambaye ana tatizo na kila mtu, huwezi kuishi katika kitongoji chochote kwa $ 81,000 sawa na T sh milioni 188 kwa mwaka sio pesa nyingi. Huwezi kuishi popote. Unazungumza juu ya mtu ambaye ana beef na kila mtu kwenye tasnia, huwezi kuishi popote.”

Choke No Joke aliingilia kati kwa kumwambia Marquise ikiwa baba yake anaweka $6,700 yaani milioni 15 za Kitanzania kwa mwezi katika malipo ya msaada wa mtoto, basi mama yake pia Shaniqua Tompkins, anapaswa kujumuisha nusu nyingine, na kufanya jumla ya malipo ya kila mwezi ya mtoto kuwa $13,400. zaidi ya milioni 30.

Choke alisema kuwa Tompkins yaani mama yake pia anastahili kuwajibika kumtunza mwanawe , lakini Marquise aliendelea kudai kuwa pesa hizo hazimtosha. kuishi katika jiji la New York.

Choke alimwambia mtoto huyo wa 50 Cent kuwa “lazima uache kulinganisha watu, Unajilinganisha na wewe kaka. Unalinganisha na kiwango chako cha maisha. Huwezi kufanya hivyo.”

Aliongeza,

“Ninajua jinsi unavyohisi kutokuwa na kitu, mfano mimi Niliondoka  kwenye nyumba yangu iliyoungua nilibaki Sina kitu.imagine Ilinibidi nijenge upya maisha yangu kwa $6700 hiyo hiyo ambayo unaiona ndogo kwa mwezi.”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents