Muigizaji wa filamu za Harry Porter, Alan Rickman afariki dunia
Muigizaji mahiri wa Uingereza, Alan Rickman aliyejipatia umaarufu kwenye filamu za Harry Porter amefariki dunia akiwa na miaka 69.
Amefariki Alhamis hii akiwa amezungukwa na familia na marafiki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.
Muigizaji huyo alikuwa akijulikana kama Professor Snape kwenye filamu za Harry Potter.
Muigizaji mkuu wa filamu hiyo, Daniel Radcliffe amemuelezea Rickman kama ‘mmoja wa waigizaji wazuri niliowahi kufanya nao kazi” pamoja na “miongoni mwa watu waaminifu na wanaosaidia wenzao niliowahi kukutana nao kwenye tasnia ya filamu.”
JK Rowling, aliyeandika vitabu vya Harry Potter alisema: There are no words to express how shocked and devastated I am to hear of Alan Rickman’s death. He was a magnificent actor & a wonderful man” huku Michael Gambon, aliyeigiza kama Dumbledore, akisema Everybody loved Alan. He was always happy and fun and creative and very, very funny.”