Burudani

Muimbaji ‘Valle Wele’ anayekuja kuleta upinzani kwenye muziki wa R&B

Kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kinaendelea kukuwa kwa kasi kila kukicha kutokana na wasanii kuendelea kufanya vizuri huku nao wasanii wachanga wakionyesha kuja kwa kasi zaidi na kuonyesha hali ya kuwa na shauku kubwa zaidi ya kufanya vizuri kuliko hata wasanii ambao wapo kwenye game.

https://youtu.be/raOi9RyxAQ4

Hayo yamedhiirishwa na msanii mpya wa muziki wa R&B, Valle Wele ambaye anaonekana kuwa na uwezo wa juu katika muziki wake.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Valle amesema anaamini anafanya muziki mzuri ambao kila mtanzania atakayepata muda wa kusiikiliza ataendelea kuufutilia muziki wake kwa kuwa ni mzuri.

“Kuna wasanii wengi wanafanya vizuri na mimi nawakubali na pia naheshimu vitu wanavyofanya, lakini mimi pia kuna kitu kizuri ambacho nafanya, naomba kila mtanzania apate fursa ya kukisikiliza na bila shaka atakuwa shabiki wangu kwa sababu naamini nafanya muziki nzuri sana,” alisema Valle

Aliongeza, “Kwa sasa nimeachia collection ya nyimbo zangu 5 kupitia mtandao wa Youtube, ni ngoma kali na nimeachia 5 kwa sababu nataka mashabiki wa muziki wangu waangalie ni kitu gani anaweza kufanya, uwezo wangu. Kwahiyo mimi nawaomba mashabiki wa muziki wapate nafasi ya kusikiliza ngoma hizo kwa sababu ni ngoma kali lakini pia nawaahidi ngoma nyingi zaidi na kali,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents