Burudani
Mwana FA: Nilimtumia tena Bosco kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye Mfalme
Rapper wa ‘Kiboko Yangu’, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amedai kuwa aliamua kumtumia tena muongozaji wa video wa nchini Kenya, Kelvin Bosco Jr kuongoza video ya ‘Kiboko Yangu’, ili kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye video ya Mfalme iliyoongozwa na muongozaji huyo pia.
“Kwa kiwango kikubwa video ya ‘Mfalme’ haikufika kwenye satisfaction zetu wote wawili yaani kama tulikuwa tunahisi kuna vitu tungeweza kuvifanya vizuri zaidi,” Mwana FA ameiambia Bongo5.
“Tukaona kwamba tusipoteze hiyo ari na video inayofuata apewe yeye tena ili tujaribu kurekebishe tupate kitu kizuri zaidi.”
Video ya wimbo huo aliomshirikisha Alikiba ilifanyika nchini Kenya na imepokelewa vizuri na mashabiki wa FA tofauti na ilivyokuwa video ya Mfalme.