Habari

Mwanamke apigana na Simba kumuokoa mumewe

Susan, Mwanamke aliyegonga vichwa vya habari baada ya kupigana na Simba kwa ujasili kuokoa maisha ya mumewe, huko Isiolo nchini Kenya.

Tukio hilo lilitokea wakati wanandoa hao wakienda kutafuta kuni na mambo kubadilika wakijikuta wanapambana na mnyama huyo hatari.

Simba huyu aliyekuwa amejificha kwenye majani alimvizia mumewe, Michael akamrukia na kumwangusha chini,  kutokana na hofu ya mara ya kwanza alikimbia alisema ni mapenzi yake kwa mume wake ndiyo yalimpa ujasiri wa kurudi kupambana na mnyama huyo.

Susan ambaye ni mama wa mtoto mmoja anasema “Juu ya upendo niliona nisiachilie huyo mnyama amle Nampenda mume wangu tena sana”.

“Hatukuwa tunatarajia, mzee alikuwa mbele mimi nilikuwa nyuma Simba huyo akamng’ata mguu na mkono, aliishiwa nguvu nikachukua panga nikamkata huyo Simba ndipo alipoanza kunigeukia, ndio Mzee akapata nafasi ya kuamka na kuanza kumkata kata simba huyo lakini hakuwa anasikia, sasa mzee alimkata mgongo ndio akaanguka chini”. alisema Susan.

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents