Michezo

Dube kamwaga Mboga Azam

“Kama nilivyosema nilipokuja hapa nilikuwa na malengo na matumaini kwa time nilidhani kua ni timu “KUBWA” ambayo ingeweza kushindana na wasifu wangu ungeongezeka zaidi.

“Wasifu wangu ulianza kushuka niliendelea kujisemea kua mambo yatakuwa mazuri lakini kila mara mambo yalikua yanaenda kuta abaya zaidi, unaweza kuona tunaanza msimu vizuri lakini katikati kila kitu kinakuwa kama misimu iliyopita” alisema Dube.

Aliendelea na kusema “kama mchezaji unahitaji kushinda “MAKOMBE” unatamani kushindana, dhamira yangu ni kucheza ndani ya Afrika na Ulaya”.

‘Kwenye timu mnaanza msimu matumaini yakiwa makubwa lakini mnaanza kupoteza na hakuna anaejali, natamani kupata changamoto mpya kwenye mazingira mapya kujaribu vitu vingine, kucheza sehemu yenye pressure kubwa na kuona namna mambo yanavyo kwenda mbele”.

 

“Kuna Viongozi (Azam FC) wako kwenye timu, lakini mioyo yao iko kwenye timu zingine wanazozipenda na time hizo zikishinda wanafurahia, hili ni tatizo jingine unajua mara nyingine ni ngumu kusema vitu vivi, lakini sasa tuko kwenye hali ngumu natakiwa kusema sina chaguo”.

“Siwezi kuwa kwenye timu ambayo wewe unataka kushinda kitu, lakini yatu ambao wanaowaongoza wanasapoti timu mnazoshindana nazo, nido maana nataka mabadiliko niwe sehemu ambayo watu wanaowaongoza mnafikiria kimoja”.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents