Burudani

RECAP: Nandy alimdhulumu Jay Melody?? Kwanini analalamika (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia malalamiko aliyoyatoa Jay Melody.

Jay Melody akifanyiwa mahojiano na media kadhaa ameeleza kuwa amuandikia Nandy nyimbo nyingi lakini hakuwa kupata haki yake.

Jay Melody ametoa kauli iliyozua utata baada ya kusema kuwa yeye hakuwahi kumuandikia Nandy nyimbo wimbo wowote bali nyimbo zake zilikuwa zinachukuliwa bila maridhiano yoyote anapewa Nandy.

Ameongeza kuwa licha ya Nandy kupewa nyimbo hizo zilifanya vizuri lakini yeye hakupata credit yoyote akiwa kama Muandishi wa nyimbo na kusema yeye ndio kiherehere chake alikuwa akijipa maua mitandaoni.

Kauli ya Jay Melody inaonyesha bado anadai haki za nyimbo zake alizoandika na kwa kauli hiyo kuna haja ya Nandy kumaliza tofauti zao.

Unahisi kuna haja ya Nandy kukutana naye na kumalizana naye au apotezee tu?? Na Je Jay Melody bado ana haki ya kudai haki yake licha ya muda mrefu kupita??

 

Host: @el_mando_tz
Cameraman: @samirkakaa

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents