Habari

Nabii na Mtume Boniface Mwamposa, wenzake waachiwa kwa dhamana

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema watu wanane akiwemo Nabii na Mtume Boniface Mwamposa wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa kina.

Wote wanatuhumiwa kuendesha kongamano lililosababisha vifo vya watu 20 mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Mwananchi Digital, Msemaji wa Polisi David Misime amethibitisha.

Hapo juzi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Mtume na Nabii Boniface Mwamposa baada ya kutoroka mjini Moshi kufuatia vifo vya watu 20 ambao walikuwa wanakanyaga mafuta ya upako mahala alipokuwa akihubiri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents