Michezo

Nafasi ya Manchester United ni ipi kwenye ligi baada ya kuwakosa wachezaji zaidi ya 7 katika kikosi cha kwanza wakiwa ni majeruhi

Wachambuzi wana tathmini kwamba kujeruhiwa kwa wachezaji wa Manchester uniyted kunaweza kutoa nafasi na faida kwa Crystal Palace hatimaye leo kufanikiwa kushinda mechi ya ligi kuu England dhidi ya mashetani wekundu.

Ushindi wao mkubwa dhidi ya Leicester mara ya mwisho haikufua matumaini ya timu hiyo ya Wanamwewe lakini pia kuondosha hofu ya kuanguaka chini ya daraja na pengine ndio imewapatia hamu ya kuonyesha umahiri na azma ya kutafuta mabao ambayo wameyakosa msimu huu.

Kwa mujibu wa BBC. Kaimu msimamizi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer huenda akakosa wachezaji takriban 9 wa timu ya kwanza.
Ander Herrera, Anthony Martial, Jesse Lingard, Juan Mata, Phil Jones na Nemanja Matic wote inaarifiwa hawatoweza kucheza leo huku Marcus Rashford akitiliwa shaka.

Matteo Darmian na Antonio Valencia hawapo lakini Marcos Rojo anatarajiwa uwanjani.


Meneja Roy Hodgson wa Crystal Palace

Huku upande wa Crystal Palace, beki wa kati Mamadou Sakho atakosa mechi ya leo Jumatano kutokana na jeraha la goti lililomlazimu kuondoka uwanjani dhidi ya Leicester.

Walinzi wenza Martin Kelly na Aaron Wan-Bissaka watafanyiwa ukaguzi.

Wakati kikosi cha ulinzi kikiwa na udhaifu huo, Ole Gunnar Solskjaer amemuita Alexis Sanchez na Romelu Lukaku kuingia kati na kucheza kwa uwezo wao kikamilifu.


Huenda Manchester United ikakosa wachezaji takriban 9 wa timu ya kwanza

kichwa kwa kichwa

  • Crystal Palace haijafanikiwa kuishinda Manchester United katika Premier League baada ya majaribio 19.
  • Eagles imefanikiwa kufunga mabao 7 katika mechi 19.
  • Palace haijapata ushindi katika mechi 21 za ligi dhidi ya United tangu ushindi wa 3-0 mnamo Mei 1991, wakati John Salako alipofunga mabao mawili.
  • Wanajaribu kuepuka kufungwa katika mpambano wote katika muda wa msimu mmoja kwamara ya kwanza tangu 1989-90.

Kauli za wakufunzi

Meneja Roy Hodgson wa Crystal Palace : “Naitazamia mechi hiii. Nilisikitika kuipoteza mechi mwaka jana.

“Natarajia hii ikiwa mechi nzuri ya soka. Litakuwa jukumu kubwa kwetu. Wachezaji wako sawa.”

Kaimu meneja wa Manchester UnitedOle Gunnar Solskjaer kuhusu majeraha :“Tutakuwana kikosi thabiti uwanjani bila shaka.

“Kutakuwana nafasi kwa wengine. Nimeketishwa nje ya uwanja na nikapata fursa wakati hali kama hii ilipojiri. Wachezaji walioingia dhidi ya Liverpool, Scott McTominay na Andreas Pereira, nadhani walicheza vizuri mno.

“Hivyo ndivyo hali ilivyo. Ni lazima uwe tayari unapoipata fursa.”

Je..! Manchester United itafanikiwa kuingia top four, na je kwenye klabu bingwa bari Ulaya dhidi ya PSG na vipi kuhusu FA….?

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents