Michezo

Nafasi ya vilabu vya Uingereza ni ipi katika michuano mikubwa barani Ulaya baada ya Arsenal na Chelsea kufanya vizuri, Liverpool nao na Tottenham kutinga nusu fainali UEFA

Nafasi ya vilabu vya Uingereza ni ipi katika michuano mikubwa barani Ulaya baada ya Arsenal na Chelsea kufanya vizuri, Liverpool nao na Tottenham kutinga nusu fainali UEFA

Katika hali isiyo ya kawaida vilabu ya Uingereza mwaka huu vimeamua kweli kweli katika michuano mikubwa barani Ulaya UEFA , kwani mpaka hivi sasa Liverpool na Tottenham vimetingaa hatua ya nusu fainali katika michuano ya UEFA lakini kwa bahati mbaya vikapata matokeo mabaya katika michezo yao yamwanzo ya hatua hiyo kwani Tottenham wao walipoteza kwa goli moja dhidi ya Ajax kutoka nchni Uholanzi ingawa walikuwa nyumbani mjini London na kwa upande wa Liverpool wakienda kuanzia ugenini dhidi ya wababe wa katalunya FC Barcelona nao wakapoteza kwa jumla ya goli 3 kwa 0 ingawa bado kuna mchezo wa marudiano.

Na katika UEFA ndogo yaani UEFA Europe League vilabu vingine kutoka Uingereza Arsenal na Chelsea nao walipata matokeo ya kuridhidsha usiku wa leo.

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette alofunga magoli mawili huku Sarsenal ikitoka nyuma katika uwanja wa Emirates na kuilaza valencia katika mechi ya mkodo wa kwanza ya nusu fainali ya Europa League.

Mouctar Diakhaby aliiweka mbele valencia kupitia kichwa kilichomuwacha bila Jibu Petr Cech kabla ya Lacazette kusawazisha kutoka kwa pasi iliotolewa na Pierre-Emerick Aubameyang.

Baadaye mshambuliaji huyo wa Ufaransa alifunga goli la pili kutoka kwa krosi iiliopigwa na Granit Xhaka dakika saba baadaye na kufanya mambo kuwa 7-1 kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Alexander lacazette akicheka na wavu dhidi ya ValenciaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mkufunzi wa Arsenal Unai EmeryHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Na goli la mwisho la Aubameyang katika dakika za lala salama ziliihakikishia ushindi Arsenal wa mabao mawili kabla ya mkondo wa pili wa mchuano huo utakaochezwa Uhispania.

Wakati huo huo Chelsea ilitoka sare ya 1-1 katika mechi nyengine ya nusu fainali ya Europa baada ya kiungo wa kati wa Chelsea Pedro kuipatia timu yake bao la Ugenini.

Chelsea dhidi ya Eintracht Franfurt ya Ujerumani katika nusu fainali ya EUROPA LEAGUEHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Eintracht Franfurt ilichukua uongozi kupitia mshambuliaji Luka Jovic ambaye alipata pasi nzuri kutoka kwa Filip Kostic.

The Blues ambao walianza na Eden hazard akiwa mchezaji wa ziada walisawazisha wakati Pedro alifunga goli zuri kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Beki David Luiz pia alikosa bao pale mkwaju wake wa adhabu uligonga mwamba wa goli.

Pedro aliifungia Chelsea bao la ugeniniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Sare hiyo inamaanisha kwamba Chelsea itakuwa timu ya kwanza kucheza mechi 16 za Europa League bila kushindwa , ikivunja rekodi iliowekwa na Atletico Madrid kutoka 2011 hadi 2012.

Watakuwa na fursa ya kuimarisha rekodi hiyo hadi mechi 17 Alhamisi ijayo katika mkondo wa pili nchini Uingereza.

Katika mechi ya Arsenal Lacazette angejipatia hat-trick yake ya kwanza baaa ya kukosa bao la wazi kutoka maguu sita ya goli katika kipindi cha pili na baadaye akazuiliwa na kipa Neto katika visa viwili.

Arsenal sasa itaelekea Valencia kwa awamu ya pili siku ya Alhamisi wakitumai kuzuia kushindwa kwa nusu fainali yao ya pili baada ya kuondolewa na Ateltico madrid mwaka uliopita.

Baada ya matokeo hayo inaonyesha namna gani vilabu hivi vilivyopambana mwaka huu kupeleka vilabu vinne katika hatua ya nusu fainali ya michuano mikubwa ya UEFA barani Ulaya lakini swali ni je vitaweza kuondoka na moja ya taji mwaka huu au vitaacha mataji yote…?

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents