Burudani

Ngoma mpya ya Jux ‘Sisikii’ imeandikwa na Mabeste

Mabeste ni rapper anayefahamika kwa uwezo wake mkubwa kiuandishi lakini kitu ambacho wengi hawakifahamu ni kuwa hitmaker huyo wa ‘Baadaye Sana’ ni producer na mwandishi mzuri wa nyimbo.

Mabeste akitumbuiza

Katika kuthibitisha hilo, msanii huyo wa zamani wa B’Hits ameuandika wimbo mpya wa Jux unaotoka leo, Sisikii.

February mwaka huu, rapper huyo aliiambia Bongo5 ameanzisha timu itakayokuwa inahusika na utunzi, uandishi na utayarishaji wa nyimbo za wasanii mbalimbali.

“Sasa hivi ntakuwa natengeneza instrumental za nyimbo za kuimba, halafu natafuta artist wa kuimba, namweka ndani anaimba. Kwahiyo ile ngoma ikitoka itakuwa ni producer wa instrumental ni Mabeste, mwandishi Mabeste halafu masuala ya mixing na mastering mtu mwingine,”Mabeste aliiambia Bongo5.

“Kwahiyo ntakuwa nauza package kwa design hiyo. Kwa mfano kama Ben Pol ni msanii wa R&B, naandika nyimbo za R&B nazicompose kila kitu, kwahiyo mimi namtumia nyimbo ambayo tayari ina maneno yake kila kitu, akipenda navua maneno yangu, anakariri yale maneno inatoka nyimbo.”

Mabeste amesema tayari kwa sasa kwenye timu yake anaye mwandishi mmoja pamoja na producer mmoja, na yeye mwenyewe. “Nataka kuongeza producer mmoja tuwe watatu na waandishi watatu. Tunakuwa ni timu fulani ambayo tunaunda music halafu tunawauzia watu package nzima.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents