Burudani

Nick wa Pili aeleza kwanini wimbo wake mpya ‘Baba Swalehe’ umekuwa gumzo mapema

Rapper wa kundi la Weusi, Nick wa Pili amesema wimbo wake mpya ‘Baba Swalehe’ umekuwa gumzo mapema kutokana na ujumbe wake na jinsi alivyobadilika kwenye aina ya uchanaji.

10475068_580578882090207_1870253540_n

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo utakuwa ni miongoni mwa nyimbo zake zitakazoishi kwa muda mrefu zaidi.

“Kichwa cha jina la wimbo kimechangia wimbo kwenda haraka, utofauti wa kilichoimbwa, ujumbe ni wa kufurahisha sana, muundo wa chorus ni mpya, beat hata michano ni vipya ndio kitu ambacho kimewagusa watu,” amesema Nick.

“Naona pia hii ni miongoni mwa nyimbo zangu ambazo zitaishi muda mrefu kama Sitaki Kazi. Kwahiyo Baba Swalehe ni kitu ambacho kitaendelea kupendwa na kuishi miaka mingi sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents