Burudani

Nikki Wa Pili: Ni vizuri msanii ukajua njia yako ya kupita kwenye muziki

Rapper Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi, amesema ni muhimu kwa msanii kutambua aina ya muziki anaoweza kuufanya ili kuepuka kutapatapa kutaka kubadilisha aina ya muziki katikati ya safari.

Nikki-wa-pili-2233

Nikki ameiambia E-newz ya EATV kuwa, wasanii hao huimba muziki wa mapokeo bila kujua sauti gani ambazo ni nzuri kwa muziki wao.

“Ukielewa category uliopo inakujenga wewe msanii, ukatambua ok kumbe muziki ni mpana nichague njia yangu ya kupita, kwahiyo ni vizuri msanii ukajua njia yako ya kupita, itakujenga sana tena utajitambua muziki unaofanya ni muziki wa aina gani? Na unakuwa vipi? , then unaangalia wale watu kwenye categories yako wamekuwa wakienda vipi?, lakini dalili ya mwanamuziki kutokujua anafanya muziki gani, anaimba muziki wa kimapokeo, sasa mara nyingi ukiwa ni msanii wa namna hiyo, unaweza ukapotea hapo katikati, kubadilika unaweza ukabadilika ndani ya muziki wako na kuchanganya kidogo ili kupata ladha Fulani,” alisema Nikki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents